Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 32 Biblia Habari Njema (BHN)

Maondoleo ya dhambi

(Zaburi ya Daudi. Funzo)

1. Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake,mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.

2. Heri mtu ambaye Mwenyezi-Mungu hamwekei hatia,mtu ambaye hana hila moyoni mwake.

3. Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu,nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.

4. Mchana na usiku mkono wako ulinilemea;nikafyonzwa nguvu zangu,kama maji wakati wa kiangazi.

5. Kisha nilikiri makosa yangu kwako;wala sikuuficha uovu wangu.Nilisema ninakuungamia makosa yangu ee Mwenyezi-Mungu,ndipo nawe ukanisamehe dhambi zangu zote.

6. Kwa hiyo, kila mwaminifu na akuletee maombi;jeshi likaribiapo au mafuriko,hayo hayatamfikia yeye.

7. Wewe ndiwe kinga yangu;wewe wanilinda katika taabu.Umenijalia shangwe za kukombolewa.

8. Mungu asema: “Nitakufunzana kukuonesha njia unayopaswa kufuata.Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.

9. Usiwe mpumbavu kama farasi au nyumbu,ambao lazima wafungwe lijamu na hatamu,la sivyo hawatakukaribia.”

10. Watu waovu watapata mateso mengi,bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.

11. Furahini na kushangilia kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu;pigeni vigelegele vya shangwe enyi wanyofu wa moyo.