Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 2 Biblia Habari Njema (BHN)

Mfalme mteule wa Mungu

1. Kwa nini mataifa yanafanya ghasia?Mbona watu wanafanya njama za bure?

2. Wafalme wa dunia wanajitayarisha;watawala wanashauriana pamoja,dhidi ya Mwenyezi-Mungu na mteule wake.

3. Wanasema: “Tujiondoe katika utawala wao;tutupilie mbali minyororo yao!”

4. Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni,anawacheka na kuwadhihaki.

5. Kisha, anawakaripia kwa ghadhabu,na kuwatisha kwa hasira, akisema:

6. “Nimemtawaza mfalme niliyemteua,anatawala Siyoni, mlima wangu mtakatifu!”

7. Mfalme asema: “Nitatangaza azimio la Mwenyezi-Mungu.Mungu aliniambia:‘Wewe ni mwanangu,mimi leo nimekuwa baba yako.

8. Niombe nami nitakupa mataifa yawe urithi wako,na dunia nzima kuwa mali yako.

9. Utawaponda kwa fimbo ya chuma;utawavunja kama chungu cha mfinyanzi!’”

10. Sasa enyi wafalme, tumieni busara;sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia.

11. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji;

12. msujudieni na kutetemeka;asije akakasirika, mkaangamia ghafla;kwani hasira yake huwaka haraka.Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!