Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 1 Biblia Habari Njema (BHN)

KITABU CHA KWANZA

Furaha ya kweli

1. Heri mtu asiyefuata shauri la waovu,asiyeshiriki njia za wenye dhambi,wala kujumuika na wenye dharau;

2. bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu,na kuitafakari mchana na usiku.

3. Huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito,unaozaa matunda kwa wakati wake,na majani yake hayanyauki.Kila afanyalo hufanikiwa.

4. Lakini waovu sivyo walivyo;wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5. Kwa hiyo watu waovu wataanguka wakati wa hukumu,wenye dhambi hawatakaa na kusanyiko la waadilifu.

6. Maana Mwenyezi-Mungu huziongoza njia za waadilifu;lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi.