Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 39 Biblia Habari Njema (BHN)

Binadamu mbele ya Mungu

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi)

1. Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu,nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu.Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”

2. Nilikuwa kama bubu, bila kusema kitu,nilinyamaza lakini sikupata nafuu.Mateso yangu yalizidi kuwa makali,

3. mahangaiko yangu yakaniunguza moyoni.Kadiri nilivyowaza ndivyo nilivyotaabika,kisha maneno haya yakanitoka:

4. “Ee Mwenyezi-Mungu, unijulishe mwisho wangu,siku zangu za kuishi zimenibakia ngapi,nijue yapitavyo kasi maisha yangu!”

5. Kumbe umenipimia maisha mafupi sana!Maisha yangu si kitu mbele yako.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!

6. Kweli, kila mtu anapita kama kivuli;jitihada zake zote ni bure tu;anakusanya mali, asijue atakayeipata!

7. Na sasa, ee Bwana, ninatazamia nini?Tumaini langu ni kwako wewe!

8. Uniokoe katika makosa yangu yote;usikubali wapumbavu wanidhihaki.

9. Niko kama bubu, sisemi kitu,kwani wewe ndiwe uliyetenda hayo.

10. Usiniadhibu tena;namalizika kwa mapigo yako.

11. Unapomwadhibu mtu dhambi zake kwa kumkemea,unaharibu kama nondo kile akipendacho.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!

12. Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu;usikilize kilio changu,usikae kimya ninapolia.Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye,ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.

13. Uache kunitazama nipate kufurahi kidogo,kabla sijaaga dunia, na kutoweka kabisa.