Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 41 Biblia Habari Njema (BHN)

Sala ya mgonjwa

(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)

1. Heri mtu anayewajali maskini;Mwenyezi-Mungu atamwokoa wakati wa shida.

2. Mwenyezi-Mungu atamlinda na kumweka hai,naye atafanikiwa katika nchi;Mungu hatamwacha makuchani mwa maadui zake.

3. Mwenyezi-Mungu atamsaidia awapo mgonjwa,atamponya maradhi yake yote.

4. Nami nilisema: “Unifadhili, ee Mwenyezi-Mungu,unihurumie maana nimekukosea wewe.”

5. Madui zangu husema vibaya juu yangu:“Atakufa lini na jina lake litoweke!”

6. Wanitembeleapo husema maneno matupu;wanakusanya mabaya juu yangu,na wafikapo nje huwatangazia wengine.

7. Wote wanichukiao hunongonezana juu yangu;wananiwazia mabaya ya kunidhuru.

8. Husema: “Maradhi haya yatamuua;hatatoka tena kitandani mwake!”

9. Hata rafiki yangu wa moyoni niliyemwamini,rafiki ambaye alishiriki chakula changu,amegeuka kunishambulia!

10. Ee Mwenyezi-Mungu, unionee huruma!Unipe nafuu, nami nitawalipiza.

11. Hivyo nitajua kwamba unapendezwa nami,maadui zangu wasipopata fahari juu yangu.

12. Wewe umenitegemeza kwani natenda mema;waniweka mbele yako milele.

13. Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli,tangu milele na hata milele!Amina! Amina!