Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48
  49. 49
  50. 50
  51. 51
  52. 52
  53. 53
  54. 54
  55. 55
  56. 56
  57. 57
  58. 58
  59. 59
  60. 60
  61. 61
  62. 62
  63. 63
  64. 64
  65. 65
  66. 66

Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 41 Biblia Habari Njema (BHN)

Mungu anaahidi kuisaidia Israeli

1. Mungu asema hivi:“Enyi wakazi wa mbali nyamazeni mnisikilize!Enyi mataifa jipeni nguvu;jitokezeni mkatoe hoja zenu,na tuje pamoja kwa hukumu.

2. “Nani, ila mimi, aliyemwita shujaa toka mashariki,mtu ambaye hupata ushindi popote aendako?Mimi huyatia mataifa makuchani mwake,naye huwaponda wafalme chini ya miguu yake!Upanga wake huwafanya kuwa kama vumbi,kwa upinde wake huwapeperusha kama makapi.

3. Yeye huwafuatia na kupita salama;huenda kasi kana kwamba hagusi chini.

4. Nani aliyefanya yote haya yatendeke?Ni nani aliyepanga wakati wa kila tukio?Mimi Mwenyezi-Mungu nipo tangu mwanzo,mimi nitakuwapo hata milele.

5. “Wakazi wa mbali wameona niliyotenda, wakaogopa;dunia yote inatetemeka kwa hofu.Watu wote wamekusanyika, wakaja.

6. Kila mmoja anamhimiza mwenzake akisema,‘Haya! Jipe moyo!’

7. Fundi anamhimiza mfua dhahabu,naye alainishaye sanamu kwa nyundo,anamhimiza anayeiunga kwa misumari.Wote wanasema, ‘Imeungika vizuri sana!’Kisha wanaifunga kwa misumari isitikisike.

8. “Sikiliza ewe Israeli, mtumishi wangu,wewe, Yakobo ambaye nimekuchagua,wewe mzawa wa Abrahamu, rafiki yangu;

9. wewe niliyekuleta toka miisho ya dunia,wewe niliyekuambia: ‘Wewe u mtumishi wangu;mimi sikukutupa, bali nilikuchagua.’

10. Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe.Usifadhaike, mimi ni Mungu wako.Nitakuimarisha na kukusaidia;nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.

11. “Naam! Wote waliokuwakia hasira,wataaibishwa na kupata fedheha.Wote wanaopingana nawe,watakuwa si kitu na kuangamia.

12. Utawatafuta hao wanaopingana nawe,lakini watakuwa wameangamia.

13. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,ndimi ninayetegemeza mkono wako.Mimi ndimi ninayekuambia:‘Usiogope, nitakusaidia.’”

14. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Enyi watu wa Yakobo dhaifu kama mdudu,enyi Waisraeli, msiogope!Mimi Mwenyezi-Mungu nasema nitawasaidia.Mimi ni Mkombozi wenu,Mtakatifu wa Israeli.

15. Nitawafanya muwe kama chombo cha kupuria,chenye meno mapya na makali.Mtaipura milima na kuipondaponda;vilima mtavisagasaga kama makapi.

16. Mtaipepeta milima hiyo,nao upepo utaipeperushia mbali,naam, dhoruba itaitawanya huko na huko.Nanyi mtafurahi kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu;mtaona fahari kwa sababu yanguMungu Mtakatifu wa Israeli.

17. “Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate,wakiwa wamekauka koo kwa kiu,mimi Mwenyezi-Mungu nitawajibu;mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha.

18. Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu,na chemchemi katika mabonde.Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji,na nchi kame kuwa chemchemi za maji.

19. Nitapanda miti huko nyikani:Mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni;nitaweka huko jangwani:Miberoshi, mivinje na misonobari.

20. Watu wataona jambo hilo,nao watatambua na kuelewa kwambamimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo,mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo.”

Mwenyezi-Mungu aipuuza miungu ya uongo

21. Mwenyezi-Mungu, Mfalme wa Yakobo, asema:“Enyi miungu ya mataifa,njoni mtoe hoja zenu!

22. Leteni hoja zenu, mtuambie yatakayotukia.Tuambieni matukio ya kwanza yalikuwa yapinasi tutayatafakari moyoni.Au tutangazieni yajayo,tujue yatakayokuja.

23. Tuambieni yatakayotokea baadaye,nasi tujue basi kama nyinyi ni miungu.Fanyeni kitu chochote, chema au kibaya,ili tutishike na kuogopa.

24. Hakika, nyinyi si kitu kabisa.hamwezi kufanya chochote kile.Anayechagua kuwaabudu nyinyi ni chukizo.

25. “Nimechochea mtu toka kaskazini,naye amekuja;naam, nimemchagua mtu toka mashariki,naye atalitamka jina langu.Yeye atawakanyaga wafalme kama tope,kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake.

26. Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo,hata sisi tupate kuyatambua?Nani aliyetangulia kuyatangaza,ili sasa tuseme, alisema ukweli?Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja,wala hakuna aliyesikia maneno yenu.

27. Mimi ni yule wa kwanza, niliyetangaza kwa Siyoni,nikapeleka Yerusalemu mjumbe wa habari njema.

28. Nimeangalia kwa makini sana,lakini simwoni yeyote yule;hamna yeyote kati ya hao miungu awezaye kushauri;nikiuliza hakuna awezaye kunijibu.

29. La! Miungu hiyo yote ni udanganyifu,haiwezi kufanya chochote;sanamu zao za kusubu ni upuuzi.