Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48
  49. 49
  50. 50
  51. 51
  52. 52
  53. 53
  54. 54
  55. 55
  56. 56
  57. 57
  58. 58
  59. 59
  60. 60
  61. 61
  62. 62
  63. 63
  64. 64
  65. 65
  66. 66

Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 38 Biblia Habari Njema (BHN)

Mfalme Hezekia anaugua

1. Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”

2. Hezekia akageukia upande wa ukuta na kumwomba Mwenyezi-Mungu,

3. akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi ukumbuke jinsi nilivyokutumikia kwa uaminifu na kwa moyo wangu wote, na kutenda yaliyo sawa mbele yako.” Hezekia akalia kwa uchungu sana.

4. Kisha neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Isaya:

5. “Nenda ukamwambie Hezekia, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa baba yako Daudi, anasema hivi: Nimesikia ombi lako na nimeyaona machozi yako. Basi, nakuongezea miaka kumi na mitano ya kuishi.

6. Nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mikononi mwa mfalme wa Ashuru na kuulinda.”

21. Basi, Isaya akasema, “Chukueni andazi la tini mkaliweke kwenye jipu lake, apate kupona.”

22. Hezekia akauliza, “Ni ishara gani itakayonijulisha kwamba mimi nitakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu?”

7. Isaya akamjibu, “Hii itakuwa ishara kwako kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwamba Mwenyezi-Mungu atafanya kama alivyoahidi.

8. Nitafanya kivuli kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi, kirudi nyuma hatua kumi.” Nacho kivuli kikarudi nyuma hatua kumi.

9. Kisha mfalme Hezekia alipopona, akatunga wimbo huu wa shukrani:

10. “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa,inanibidi niage dunia.Mimi nimepangiwa kwenda kuzimusiku zote zilizonibakia.

11. Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu,katika nchi ya walio hai;wala sitamwona mtu yeyote tena,miongoni mwa wakazi wa ulimwengu.

12. Makao yangu yamengolewa kwangu,kama hema la mchungaji;kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu;Mungu amenikatilia mbali;kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.

13. Usiku kucha nililia kuomba msaada;kama simba, anavunjavunja mifupa yangu;mchana na usiku ananikomesha.

14. “Ninalia kama mbayuwayu,nasononeka kama njiwa.Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu.Ee Bwana, nateseka;uwe wewe usalama wangu!

15. Lakini niseme nini:Yeye mwenyewe aliniambia,naye mwenyewe ametenda hayo.Usingizi wangu wote umenitorokakwa sababu ya uchungu moyoni mwangu.

16. “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda,kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi.Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi.

17. Nilipata mateso makali kwa faida yangu;lakini umeyaokoa maisha yangukutoka shimo la uharibifu,maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako.

18. Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe;waliokufa hawawezi kukushukuru wewe.Wala washukao huko shimonihawawezi tena kutumainia uaminifu wako.

19. Walio hai ndio wanaokushukuru,kama na mimi ninavyofanya leo.Kina baba huwajulisha watoto wao uaminifu wako.

20. “Mwenyezi-Mungu ataniokoa.Nasi tutamsifu kwa nyimbo za vinubisiku zote za maisha yetu,nyumbani kwake Mwenyezi-Mungu.”