Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48
  49. 49
  50. 50
  51. 51
  52. 52
  53. 53
  54. 54
  55. 55
  56. 56
  57. 57
  58. 58
  59. 59
  60. 60
  61. 61
  62. 62
  63. 63
  64. 64
  65. 65
  66. 66

Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 57 Biblia Habari Njema (BHN)

Onyo dhidi ya ibada za sanamu

1. Mtu mwadilifu akifa,hakuna mtu anayejali;mtu mwema akifariki,hakuna mtu anayefikiri na kusema:“Mtu huyo mwema ameondolewa asipatwe na maafa,

2. ili apate kuingia kwenye amani.”Watu wanaofuata njia ya haki,watakuwa na amani na kupumzika.

3. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Njoni hapa nyinyi wana wa wachawi;nyinyi wazawa wa wachawi, wazinzi na malaya.

4. Je, mnadhani mnamdhihaki nani?Mnamfyonya nani na kumtolea ulimi?Nyinyi wenyewe ni wahalifu tangu mwanzo,nyinyi ni kizazi kidanganyifu.

5. Nyinyi mnawaka tamaa kwenye miti ya mialoni,na katika kila mti wa majani mabichi.Mnawachinja watoto wenuna kuwatambika katika mabonde na nyufa za majabali.

6. Mnachagua mawe laini mabondeni,na kuyafanya kitovu cha maisha yenu.Mnayamiminia tambiko ya kinywajina kuyapelekea tambiko ya nafaka!Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?

7. Mmeweka vitanda vyenu juu ya milima mikubwa,na kwenda huko kutoa tambiko.

8. Nyuma ya milango na miimommetundika kinyago chenu.Nyinyi mnaniacha mimina kutandika na kuvipanua vitanda vyenu.Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao.Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya,huku mnakodolea macho kinyago chenu.

9. Mnajitia marashi na manukato kwa wingikisha mnakwenda kumwabudu Moleki.Mnawatuma wajumbe wenu huko na huko,kujitafutia miungu ya kuabudu;hata kuzimu walifika.

10. Mlichoshwa na safari zenu ndefu,hata hivyo hamkukata tamaa;mlijipatia nguvu mpya,ndiyo maana hamkuzimia.

11. “Mlimwogopa na kutishwa na nanihata mkasema uongo,mkaacha kunikumbuka mimina kuacha kabisa kunifikiria?Mimi sikuwaambia kitu kwa muda mrefu;ndio maana labda mkaacha kuniheshimu!

12. Mnafikiri mnafanya sawa,lakini nitayafichua matendo yenu,nayo miungu yenu haitawafaa kitu.

13. Mtakapolia kuomba msaada,rundo la vinyago vyenu na liwaokoe!Upepo utavipeperushia mbali;naam, pumzi itavitupilia mbali.Lakini watakaokimbilia usalama kwangu,wataimiliki nchi,mlima wangu mtakatifu utakuwa mali yao.”

Huruma ya Mungu

14. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Jengeni! Jengeni! Tayarisheni njia!Ondoeni vikwazo vyote njiani mwa watu wangu!”

15. Hivi ndivyo asemavyo Mungu aliye juu kabisa,aishiye milele na ambaye jina lake ni “Mtakatifu”:“Mimi nakaa huko juu, mahali patakatifu,nakaa pia na wenye majuto na wanyenyekevu.Mimi nitawatia moyo walio wanyenyekevuna kuwapa nguvu wenye majuto.

16. Maana sitaendelea kuwalaumuwala kuwakasirikia daima.La sivyo hao niliowaumba watadhoofika mbele yangu,nami ndiye niliyewapa pumzi yangu ya uhai.

17. Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao;niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika.Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.

18. Niliiona mienendo yao, lakini nitawaponya;nitawaongoza na kuwapa faraja,nitawatuliza hao wanaoomboleza.

19. Mimi nitawapa amani,amani kwa walio mbali na walio karibu!Mimi nitawaponya.

20. Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka,ambayo haiwezi kutulia;mawimbi yake hutupa tope na takataka.”

21. Mungu wangu asema hivi:“Watu waovu sitawapa amani.”