Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48
  49. 49
  50. 50
  51. 51
  52. 52

Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 6 Biblia Habari Njema (BHN)

Yerusalemu imezingirwa na maadui

1. Enyi watu wa Benyamini,ondokeni Yerusalemu mkimbilie usalama!Pigeni tarumbeta mjini Tekoa;onesheni ishara huko Beth-hakeremu,maana maafa na maangamizi makubwayanakuja kutoka upande wa kaskazini.

2. Mji wa Siyoni ni mzuri na mwororo,lakini utaangamizwa.

3. Watu wataujia kama wachungaji na makundi yao,watapiga hema zao kuuzunguka kila mmoja sehemu yake,wapate kuyaongoza makundi yao.

4. Watasema: “Jitayarisheni kuushambulia Siyoni.Haya! Tuanze kushambulia adhuhuri!Bahati mbaya; jua linatua!Kivuli cha jioni kinarefuka.

5. Basi, tutaushambulia usiku;tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”

6. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Kateni miti yake,rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu.Mji huu ni lazima uadhibiwe,maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.

7. Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi,ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako.Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake,magonjwa na majeraha yake nayaona daima.

8. Hilo na liwe onyo kwako ee Yerusalemu,la sivyo nitakutupa kabisa kwa chuki;nikakufanya uwe jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu.”

Watu wasiopenda kusikia

9. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobakikama watu wakusanyavyo zabibu zote;kama afanyavyo mchumazabibu,pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”

10. Nitaongea na nani nipate kumwonya,ili wapate kunisikia?Tazama, masikio yao yameziba,hawawezi kusikia ujumbe wako.Kwao neno lako, ee Mwenyezi-Mungu,limekuwa jambo la dhihaka,hawalifurahii hata kidogo.

11. Nimejaa hasira ya Mwenyezi-Mungu dhidi yao.Nashindwa kuizuia ndani yangu.Mwenyezi-Mungu akaniambia:“Imwage hasira barabarani juu ya watotona pia juu ya makundi ya vijana;wote, mume na mke watachukuliwa,kadhalika na wazee na wakongwe.

12. Nyumba zao zitapewa watu wengine,kadhalika na mashamba yao na wake zao;maana nitaunyosha mkono wangu,kuwaadhibu wakazi wa nchi hii.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

13. Wote, tangu mdogo hadi mkubwa kabisa,kila mmoja anatamani kupata faida isiyo halali.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja wao ni mdanganyifu.

14. Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu,wanasema; ‘Amani, amani’,kumbe hakuna amani yoyote!

15. Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo?La! Hawakuona aibu hata kidogo.Hawakujua hata namna ya kuona aibu.Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao;wakati nitakapowaadhibu,wataangamizwa kabisa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Israeli akataa njia ya Mungu

16. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Simameni katika njia panda, mtazame.Ulizeni mjue juu ya matukio ya zamani.Tafuteni mahali ilipo njia nzurimuifuate nanyi mtapumzisha nafsi zenu.Lakini wao wakasema:‘Hatutafuata njia hiyo.’

17. Kisha nikawawekea walinzi, nikawaambia:‘Sikilizeni ishara ya tarumbeta.’Lakini wao wakasema: ‘Hatutaisikiliza.’

18. “Kwa hiyo, sikilizeni enyi mataifa;enyi jumuiya ya watu jueni yatakayowapata.

19. Sikiliza ee dunia!Mimi nitawaletea maafa watu hawakulingana na nia zao mbaya.Maana hawakuyajali maneno yangu,na mafundisho yangu nayo wameyakataa.

20. Ya nini kuniletea ubani kutoka Sheba,na udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliki,wala tambiko zenu hazinipendezi.

21. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Tazama, nitawawekea watu hawa vikwazoambavyo vitawakwaza na kuwaangusha chini.Akina baba na watoto wao wa kiume wataangamia,kadhalika na majirani na marafiki.”

Mashambulizi kutoka kaskazini

22. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Tazameni, watu wanakuja toka nchi ya kaskazini;taifa kubwa linajitayarisha kutoka mbali duniani.

23. Wamezishika pinde zao na mikuki,watu wakatili wasio na huruma.Vishindo vyao ni kama ngurumo ya bahari.Wamepanda farasi,wamejipanga tayari kwa vita,dhidi yako ewe Siyoni!”

24. Waisraeli wanasema,“Tumesikia habari zao,mikono yetu imelegea;tumeshikwa na dhiki na uchungu,kama mwanamke anayejifungua.

25. Hatuwezi kwenda mashambani,wala kutembea barabarani;maadui wameshika silaha mikononi,vitisho vimejaa kila mahali.”

26. Mwenyezi-Mungu asema,“Jivikeni mavazi ya gunia, enyi watu wanguna kugaagaa katika majivu.Ombolezeni kwa uchungu,kama mtu anayemwombolezea mwana wa pekee,maana mwangamizi atakuja,na kuwashambulia ghafla.

27. Yeremia, wewe nimekuweka kuwa mchunguzina mpimaji wa watu wangu,ili uchunguze na kuzijua njia zao.

28. Wote ni waasi wakaidi,ni watu wanaopitapita wakisengenya wengine,wagumu kama shaba nyeusi au chuma;wote hutenda kwa ufisadi.

29. Mifuo inafukuta kwa nguvu,risasi inayeyukia humohumo motoni;ni bure kuendelea kuwatakasa watu wangu,waovu hawawezi kuondolewa uchafu wao.

30. Wataitwa ‘Takataka za fedha’,maana mimi Mwenyezi-Mungu nimewakataa.”