Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 31 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Nimejifunga rasmi mimi mwenyewe,macho yangu yasimtazame msichana kwa tamaa.

2. Au je, nangojea nini kutoka kwa Mungu aliye juu?Mungu Mwenye Nguvu ameniwekea kitu gani?

3. Je, maafa hayawapati watu waovuna maangamizi wale watendao mabaya?

4. Je, Mungu haoni njia zangu,na kujua hatua zangu zote?

5. “Kama nimeishi kwa kufuata uongo,kama nimekuwa mbioni kudanganya watu,

6. Mungu na anipime katika mizani ya haki,naye ataona kwamba sina hatia.

7. Kama hatua zangu zimepotoka,moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu;kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi,

8. jasho langu na liliwe na mtu mwingine,mazao yangu shambani na yangolewe.

9. “Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu,kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu,

10. basi, mke wangu na ampikie mume mwingine,na wanaume wengine wamtumie.

11. Jambo hilo ni kosa kuu la jinai,uovu ambao hakimu lazima atoe adhabu.

12. Kosa langu lingekuwa kama moto,wa kuniteketeza na kuangamiza,na kuchoma kabisa mapato yangu yote.

13. Kama nimekataa kesi ya mtumishi wanguwa kiume au wa kike,waliponiletea malalamiko yao,

14. nitafanya nini basi Mungu atakaponikabili?Je, akinichunguza nitamjibu nini?

15. Maana Mungu ndiye aliyeniumba mimi na mtumishi wangu;yeye ndiye aliyetuumba sisi wote.

16. “Je, nimepata kumnyima maskini mahitaji yakeau kuwafanya wajane watumaini bure?

17. Je, nimekula chakula changu peke yangu,bila kuwaachia yatima nao wapate chochote?

18. La! Tangu ujana wangu nimekuwa mlezi wao,tangu utoto wangu nimewaongoza wajane.

19. Je, nilimwona mtu anakufa kwa kukosa nguo,au maskini ambaye hana nguo ya kuvaa,

20. bila kumpa joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo wangunaye akanitakia baraka za shukrani ya moyo?

21. Kama nimenyosha mkono mahakamani dhidi ya yatima,nikijua nitapendelewa na mahakimu,

22. basi, bega langu na lingoke,mkono wangu na ukwanyuke kiwikoni mwake.

23. Maana maafa kutoka kwa Mungu ni kitisho kwangu;mimi siwezi kuukabili ukuu wake.

24. “Je, tumaini langu nimeliweka katika dhahabu,au, nimeiambia dhahabu safi, ‘Wewe ni usalama wangu?’

25. Je, nimepata kufurahia wingi wa utajiri wanguau kujivunia mapato ya mikono yangu?

26. Kama nimeliangalia jua likiangaza,na mwezi ukipita katika uzuri wake,

27. na moyo wangu ukashawishika kuviabudu,nami nikaibusu mikono yangu kwa heshima yake,

28. huo pia ungekuwa uovu wa kuadhibiwa na mahakimumaana ningekuwa mwongo mbele ya Mungu aliye juu.

29. “Je, nimefurahia kuangamia kwa adui yangu,au kufurahi alipopatwa na maafa?

30. La! Sikuruhusu kinywa changu kumtakia mabaya,kwa kumlaani ili afe.

31. Watumishi wangu wote wanasema wazikila mgeni amekaribishwa nyumbani mwangu.

32. Msafiri hakulala nje ya nyumba yangu,nilimfungulia mlango mpita njia.

33. Je nimeficha makosa yangu kama wengine?Je nimekataa kukiri dhambi zangu?

34. Sijaogopa kusimama mbele ya umati wa watu,wala kukaa kimya au kujifungia ndani,eti kwa kuogopa kutishwa na dharau zao.

35. Laiti angekuwapo mtu wa kunisikiliza!Naweza kutia sahihi yangu katika kila nilichosema.Namwambia Mungu Mwenye Nguvu anijibu!Laiti mashtaka wanayonitolea maadui zangu yangeandikwa!

36. Ningeyavaa kwa maringo mabeganina kujivisha kichwani kama taji.

37. Ningemhesabia Mungu kila kitu nilichofanya,ningemwendea kama mwana wa mfalme.

38. Kama nimeiiba ardhi ninayoilima,nikasababisha mifereji yake iomboleze,

39. kwa kufaidika na mazao yake bila kulipana kusababisha kifo cha wenyewe,

40. basi miiba na iote humo badala ya ngano,na magugu badala ya shayiri.”Mwisho wa hoja za Yobu.