Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 25 Biblia Habari Njema (BHN)

Jibu la Bildadi

1. Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:

2. “Mungu ni mwenye uwezo mkuu,watu wote na wamche.Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni.

3. Nani awezaye kuhesabu majeshi yake?Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake?

4. Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu?Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi?

5. Kwake Mungu, hata mwezi haungai vya kutosha;nyota nazo si safi mbele yake;

6. sembuse mtu ambaye ni mdudu,binadamu ambaye ni buu tu!”