Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42

Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 21 Biblia Habari Njema (BHN)

Jibu la Yobu

1. Kisha Yobu akajibu:

2. “Sikilizeni kwa makini maneno yangu;na hiyo iwe ndiyo faraja yenu.

3. Nivumilieni, nami nitasema,na nikisha sema endeleeni kunidhihaki.

4. Je, mimi namlalamikia binadamu?Ya nini basi, nikose uvumilivu?

5. Niangalieni, nanyi mshangae,fumbeni mdomo kwa mkono.

6. Nikifikiri yaliyonipata nafadhaikanafa ganzi mwilini kwa hofu.

7. Kwa nini basi waovu wanaishi bado?Mbona nguvu zao zaongezeka hata uzeeni?

8. Huwaona watoto wao wakifanikiwa;na wazawa wao wakipata nguvu.

9. Kwao kila kitu ni salama bila hofu;wala kiboko cha Mungu hakiwafikii.

10. Naam, ng'ombe wao wote huongezeka,huzaa bila matatizo yoyote.

11. Watoto wao wachanga huwatembeza kama kundi;na watoto wao hucheza ngoma;

12. hucheza muziki wa ngoma na vinubi,na kufurahia sauti ya filimbi.

13. Huishi maisha ya fanakakisha hushuka kwa amani kuzimu.

14. Humwambia Mungu, ‘Usitusumbue!Hatutaki kujua matakwa yako.

15. Mungu Mwenye Nguvu ni nini hata tumtumikie?Tunapata faida gani tukimwomba dua?’

16. Kufanikiwa kwao si kuko mikononi mwao,wakiwa wamemweka Mungu mbali na mipango yao?

17. “Mara ngapi umepata kuona mwanga wa maisha ya mwovu umezimwa,wakapata kukumbwa na maafa,au Mungu amewahi kuwaangamiza kwa hasira yake?

18. Hata hivyo, na wapeperushwe kama majani makavu,wawe kama makapi yanayochukuliwa na dhoruba!

19. “Nyinyi mwasema, ‘Mungu amewawekea watoto waoadhabu ya watu hao waovu.’Kwa nini hawalipizi wao wenyewe, wapate kutambua!

20. Waone wao wenyewe wakiangamia;waone wenyewe ghadhabu ya Mungu mwenye nguvu.

21. Maana wakifa watajali nini juu ya wazawa wao,wakati siku zao zitakapokuwa zimefika mwisho?

22. Je, binadamu aweza kumfunza Mungu maarifa,Mungu ambaye huwahukumu wakazi wa mbinguni?

23. “Mtu hufa katika kilele cha ufanisi wake,akiwa katika raha mustarehe na salama;

24. amejaa mafuta tele mwilini,na mifupa yake ikiwa bado na nguvu.

25. Mwingine hufa na huzuni kubwa moyoni,akiwa hajawahi kuonja lolote jema.

26. Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa,wote hufunikwa na mabuu.

27. “Sikilizeni! Mimi nayajua mawazo yenu yote,na mipango yenu ya kunidharau.

28. Eti mwauliza, ‘Iko wapi nyumba ya mkuu?Iko wapi nyumba alimoishi mwovu?’

29. “Je, hamjawauliza wapita njia,mkakubaliana na ripoti yao?

30. Mwovu husalimishwa siku ya maafa,huokolewa siku ya ghadhabu!

31. Ni nani atakayemshutumu mtu mwovu,au atakayemlipa kwa yote aliyotenda?

32. Anapochukuliwa kupelekwa kaburini,kaburi lake huwekewa ulinzi.

33. Watu wengi humfuata nyumana wengine wengi sana humtangulia.Anapozikwa, udongo huteremshwa taratibu.

34. Mtawezaje basi, kunifariji kwa maneno matupu?majibu yenu hayana chochote ila uongo.”