Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 18:14-28 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Upande wa magharibi wa mlima huo ulio kusini mwa Beth-horoni mpaka uligeuka ukaelekea kusini hadi Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, mji ambao ni mali ya kabila la Yuda. Huu ndio uliokuwa mpaka wake upande wa magharibi.

15. Upande wa kusini mpaka wake ulianzia kwenye viunga vya mji wa Kiriath-yearimu, ukafika Efroni na kwenda hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa.

16. Kisha ulielekea chini kupitia pembeni mwa mlima ulioko karibu na bonde la mwana wa Hinomu, ambalo lilikuwa katika sehemu ya kaskazini zaidi ya bonde la Warefai. Halafu mpaka uliteremka kuelekea bonde la Hinomu, kusini mwa kilima cha Wayebusi, ukaendelea kuteremka hadi En-rogeli.

17. Huko, mpaka uligeuka kwenda kaskazini kuelekea En-shemeshi, ukapitia Gelilothi unaokabili mwinuko wa Adumimu na kuteremka hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.

18. Kutoka hapo, mpaka ulizunguka kaskazini kwenye ukingo wa juu wa Araba na kuishia huko Araba.

19. Tena, ukaendelea kwa upande wa kaskazini wa kilima cha Beth-hogla na kuishia kaskazini kabisa ya ghuba ya Bahari ya Chumvi, mahali unapoingilia mto Yordani. Huu ni mpaka wake kwa upande wa kusini.

20. Mto Yordani ndio uliokuwa mpaka wake upande wa mashariki. Ndivyo zilivyowekewa mipaka nchi zilizopewa koo za kabila la Benyamini.

21. Miji ya koo za kabila la Benyamini ni Yeriko, Beth-hogla, Emek-kesisi,

22. Beth-araba, Zemaraimu, Betheli,

23. Avimu, Para, Ofra,

24. Kefar-amoni, Ofni na Geba. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

25. Miji mingine ni Gibeoni, Rama, Beerothi,

26. Mizpa, Kefira, Moza,

27. Rekemu, Irpeeli, Tarala,

28. Zela, Ha-elefu, Yebusi, yaani Yerusalemu, Gibea na Kiriath-yearimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu waliyopewa watu wa kabila la Benyamini na koo zao.

Kusoma sura kamili Yoshua 18