Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 8:14-22 Biblia Habari Njema (BHN)

14. “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa?Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome,tukaangamie huko!Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie,ametupa maji yenye sumu tunywe,kwa kuwa tumemkosea yeye.

15. Tulitazamia kupata amani,lakini hakuna jema lililotokea.Tulitazamia wakati wa kuponywa,badala yake tukapata vitisho.

16. Sauti za farasi wao zinasikika,kwa mlio wa farasi wao wa vita,nchi nzima inatetemeka.Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo,kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.

17. “Basi nitawaleteeni nyoka;nyoka wenye sumu wasioweza kurogwa na walozi,nao watawauma nyinyi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

18. Huzuni yangu haiwezi kutulizwa,moyo wangu wasononeka ndani yangu.

19. Sikiliza kilio cha watu wangu,kutoka kila upande katika nchi.“Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni?Je, mfalme wake hayuko tena huko?”“Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu,na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”

20. “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha,nasi bado hatujaokolewa!

21. Jeraha la watu wangu limeniumiza moyoni,ninaomboleza na kufadhaika.

22. Je, hakuna dawa ya kupaka huko Gileadi?Je, hakuna mganga huko?Mbona basi watu wangu hawajaponywa?

Kusoma sura kamili Yeremia 8