Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 11:16-23 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Wakati fulani, mimi nilisema, wao ni mzeituni wenye majani mabichi, mzeituni mzuri na wenye matunda mema; lakini sasa, kwa ngurumo ya dhoruba kubwa, nitauchoma moto na kuyateketeza matawi yake.

17. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi niliuotesha huu mzeituni; lakini natangaza maafa dhidi yake kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirisha kwa kumfukizia ubani mungu Baali.”

18. Mwenyezi-Mungu alinijulisha, nami nikaelewa;Mwenyezi-Mungu alinijulisha njama zao.

19. Nami nilikuwa kama kondoo mpole anayepelekwa machinjoni;sikujua kuwa njama walizofanya zilikuwa dhidi yangu.Walisema: “Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake,tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,kamwe jina lake lisikumbukwe tena.”

20. Lakini, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi,wewe unayehukumu kwa haki,unayepima mioyo na akili za watu,unijalie kuona ukiwalipiza kisasi,maana kwako nimekiweka kisa changu.

21. Ndiyo maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anacho cha kusema juu ya watu wa Anathothi ambao wanataka kuniua na kuniambia: “Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi-Mungu, la sivyo tutakuua.”

22. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitawaadhibu watu hao. Vijana wao watauawa vitani; watoto wao wa kiume na wa kike watakufa kwa njaa.

23. Nimepanga muda wa kuleta maangamizi juu ya watu wa Anathothi. Wakati huo utakapofika, hakuna hata mmoja wao atakayebaki hai.”

Kusoma sura kamili Yeremia 11