Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 11:16-21 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Wakati fulani, mimi nilisema, wao ni mzeituni wenye majani mabichi, mzeituni mzuri na wenye matunda mema; lakini sasa, kwa ngurumo ya dhoruba kubwa, nitauchoma moto na kuyateketeza matawi yake.

17. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi niliuotesha huu mzeituni; lakini natangaza maafa dhidi yake kwa sababu ya maovu ambayo watu wa Israeli na Yuda wameyafanya. Wamenikasirisha kwa kumfukizia ubani mungu Baali.”

18. Mwenyezi-Mungu alinijulisha, nami nikaelewa;Mwenyezi-Mungu alinijulisha njama zao.

19. Nami nilikuwa kama kondoo mpole anayepelekwa machinjoni;sikujua kuwa njama walizofanya zilikuwa dhidi yangu.Walisema: “Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake,tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,kamwe jina lake lisikumbukwe tena.”

20. Lakini, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi,wewe unayehukumu kwa haki,unayepima mioyo na akili za watu,unijalie kuona ukiwalipiza kisasi,maana kwako nimekiweka kisa changu.

21. Ndiyo maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anacho cha kusema juu ya watu wa Anathothi ambao wanataka kuniua na kuniambia: “Usitoe unabii kwa jina la Mwenyezi-Mungu, la sivyo tutakuua.”

Kusoma sura kamili Yeremia 11