Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14

Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 11 Biblia Habari Njema (BHN)

Upendo wa Mungu wapita hasira yake

1. “Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,Kutoka Misri nilimwita mwanangu.

2. Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita,ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami;waliendelea kuyatambikia Mabaali,na kuvifukizia ubani vinyago vya miungu.

3. Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea!Mimi mwenyewe niliwachukua mikononi mwangu;lakini hawakutambua kuwa mimi ndiye niliyewatunza.

4. Niliwaongoza kwa kamba za hurumanaam, kwa kamba za upendo;kama baba amwinuaye mtoto mpaka shavuni mwake,ndivyo nami nilivyokuwa kwao.Mimi niliinama chini na kuwalisha.

5. Basi, watarudi nchini Misri;watatawaliwa na mfalme wa Ashuru,kwa sababu wamekataa kunirudia.

6. “Upanga utavuma katika miji yao,utavunjavunja miimo ya malango yakena kuwaangamiza katika ngome zao.

7. Watu wangu wamepania kuniacha mimi,wakiitwa waje juu,hakuna hata mmoja anayeweza.

8. Ewe Efraimu, nawezaje kukuacha?Nawezaje kukutupa ewe Israeli?Nitawezaje kukufanya kama mji wa Adma?Nitawezaje kukutenda kama Seboimu!Nazuiwa na moyo wangu;huruma yangu imezidi kuwa motomoto.

9. Nitaizuia hasira yangu kali;sitamwangamiza tena Efraimu,maana mimi ni Mungu, wala si binadamu.“Mimi ndimi Mtakatifu miongoni mwenu,nami sitakuja kuwaangamiza.

10. “Watanifuata mimi Mwenyezi-Mungu ningurumaye kama simba;nitakaponguruma watanijia toka magharibi wakitetemeka.

11. Watakuja kutoka Misri wakitetemeka kama ndege,wataruka kutoka Ashuru kama huanami nitawarudisha makwao;mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

12. Watu wa Efraimu wananirundikia uongo,na Waisraeli udanganyifu.Watu wa Yuda, wananiasi mimi Mungu Mtakatifu.