Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14

Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 10 Biblia Habari Njema (BHN)

Kuharibiwa kwa vitu vya ibada vya Israeli

1. Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri,mzabibu wenye kuzaa matunda.Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka,ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu.Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi,ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.

2. Mioyo yao imejaa udanganyifu.Sasa ni lazima wawajibike kwa hatia yao.Mwenyezi-Mungu atazibomoa madhabahu zaona kuziharibu nguzo zao.

3. Wakati huo watasema:“Hatuna tena mfalme,kwa kuwa hatumchi Mwenyezi-Mungu;lakini, naye mfalme atatufanyia nini?”

4. Wanachosema ni maneno matupu;wanaapa na kufanya mikataba ya bure;haki imekuwa si haki tena,inachipua kama magugu ya sumu shambani.

5. Wakazi wa Samaria watatetemekakwa sababu ya ndama wa huko Betheli.Watu wake watamwombolezea ndama huyo,hata makuhani wanaomwabudu watamlilia;kwani fahari ya ndama huyo imeondolewa.

6. Kinyago hicho kitapelekwa Ashuru,kama ushuru kwa mfalme mkuu.Watu wa Efraimu wataaibishwa,Waisraeli watakionea aibu kinyago chao.

7. Mfalme wa Samaria atachukuliwa,kama kipande cha mti juu ya maji.

8. Mahali pa kuabudia vilimani pa Aweni,dhambi ya Waisraeli, pataharibiwa.Miiba na magugu vitamea katika madhabahu zao.Nao wataiambia milima, “Tufunikeni”na vilima, “Tuangukieni!”

Israeli atavuna alichopanda

9. Enyi Waisraeli,nyinyi mmetenda dhambi tangu kule Gibea,na bado mnaendelea.Hakika vita vitawaangamiza hukohuko Gibea.

10. Nitawajia watu hawa wapotovu na kuwaadhibu;watu wa mataifa watakusanyika kuwashambulia,watakapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao nyingi.

11. Efraimu ni ndama aliyefundishwa vizuri,akapenda kupura nafaka.Lakini sasa shingo yake nzuri nitaifunga nira.Yuda atalima kwa jembe yeye mwenyewe,naam, Yakobo atakokota jembe la kupalilia.

12. Pandeni wema kwa faida yenu,nanyi mtavuna upendo;limeni mashamba yaliyoachwa,maana wakati wa kunitafuta mimi Bwana umefikanami nitawanyeshea baraka.

13. Lakini nyinyi mmepanda uovu,nyinyi mmevuna dhuluma;mmekula matunda ya uongo wenu.Wewe Israeli ulitegemea nguvu zako mwenyewe,na wingi wa askari wako.

14. Kwa hiyo msukosuko wa vita utawajia watu wako;ngome zako zote zitaharibiwa,kama Shalmani alivyoharibu Beth-arbeli vitani,kina mama wakapondwa pamoja na watoto wao.

15. Ndivyo itakavyokuwa kwenu enyi watu wa Betheli,kwa sababu ya uovu wenu mkuu.Kutakapopambazuka mfalme wa Israeli atawatokomeza.