Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 6:16-23 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Simameni katika njia panda, mtazame.Ulizeni mjue juu ya matukio ya zamani.Tafuteni mahali ilipo njia nzurimuifuate nanyi mtapumzisha nafsi zenu.Lakini wao wakasema:‘Hatutafuata njia hiyo.’

17. Kisha nikawawekea walinzi, nikawaambia:‘Sikilizeni ishara ya tarumbeta.’Lakini wao wakasema: ‘Hatutaisikiliza.’

18. “Kwa hiyo, sikilizeni enyi mataifa;enyi jumuiya ya watu jueni yatakayowapata.

19. Sikiliza ee dunia!Mimi nitawaletea maafa watu hawakulingana na nia zao mbaya.Maana hawakuyajali maneno yangu,na mafundisho yangu nayo wameyakataa.

20. Ya nini kuniletea ubani kutoka Sheba,na udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliki,wala tambiko zenu hazinipendezi.

21. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Tazama, nitawawekea watu hawa vikwazoambavyo vitawakwaza na kuwaangusha chini.Akina baba na watoto wao wa kiume wataangamia,kadhalika na majirani na marafiki.”

22. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Tazameni, watu wanakuja toka nchi ya kaskazini;taifa kubwa linajitayarisha kutoka mbali duniani.

23. Wamezishika pinde zao na mikuki,watu wakatili wasio na huruma.Vishindo vyao ni kama ngurumo ya bahari.Wamepanda farasi,wamejipanga tayari kwa vita,dhidi yako ewe Siyoni!”

Kusoma sura kamili Yeremia 6