Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 14:14-19 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Naye Mwenyezi-Mungu, akaniambia: “Hao manabii wanatoa unabii wa uongo kwa jina langu. Mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi yasiyo na maana yoyote, uongo wanaojitungia wenyewe.

15. Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi kuhusu hao manabii wanaotabiri kwa jina langu, ingawa mimi sikuwatuma, na wanaosema kwamba hapatakuwa na vita wala njaa katika nchi hii: Manabii hao wataangamia kwa upanga na kwa njaa.

16. Na hao ambao waliwatabiria mambo hayo, watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu wakiwa wamekufa kwa njaa na vita, wala hapatakuwa na mtu wa kuwazika. Hayo yatawapata wao wenyewe, wake zao, watoto wao wa kike na wa kiume; maana mimi nitawamwagia uovu wao wenyewe.

17. Hivi ndivyo utakavyowaambia:Laiti macho yangetoa machozi kutwa kucha,wala yasikome kububujika,maana, watu wangu wamejeruhiwa vibaya,wamepata pigo kubwa sana.

18. Nikienda nje mashambani,naiona miili ya waliouawa vitani;nikiingia ndani ya mji,naona tu waliokufa kwa njaa!Manabii na makuhani wanashughulikia mambo yao nchini,wala hawajui wanalofanya.”

19. Ee Mwenyezi-Mungu, je, umemkataa Yuda kabisa?Je, moyo wako umechukizwa na Siyoni?Kwa nini umetupiga vibaya,hata hatuwezi kupona tena?Tulitazamia amani, lakini hatukupata jema lolote;tulitazamia wakati wa kuponywa, badala yake tukapata vitisho.

Kusoma sura kamili Yeremia 14