Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 53:8-12 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa;na hakuna mtu aliyejali yanayompata.Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai,kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

9. Walimzika pamoja na wahalifu;katika kifo aliwekwa pamoja na matajiri,ingawa hakutenda ukatili wowote,wala hakusema neno lolote la udanganyifu.

10. Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumizana kumweka katika huzuni.Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi.Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa;ataishi maisha marefu.Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu.

11. Mungu asema:“Baada ya kutaabika sana,mtumishi wangu atafurahi.Kwa kuwajibika kwake kikamilifu,atatosheka na matokeo hayo.Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwadilifuatawafanya wengi wawe waadilifuYeye atazibeba dhambi zao.

12. Kwa hiyo, nitamweka katika cheo cha wakuu,atagawa nyara pamoja na wenye nguvu;kwa kuwa alijitolea mwenyewe kufa,akawekwa katika kundi moja na wakosefu,alizibeba dhambi za watu wengi,akawaombea msamaha hao wakosefu.”

Kusoma sura kamili Isaya 53