Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 53:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nani aliyeamini mambo tuliyosikia?Nani aliyetambua kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu ulihusika?

2. Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu,mtumishi wake alikua kama mti mchanga,kama mzizi katika nchi kavu.Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza,wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.

3. Alidharauliwa na kukataliwa na watu,alikuwa mtu wa uchungu na huzuni.Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu;alidharauliwa na tukamwona si kitu.

4. Hata hivyo alivumilia majonzi yetu,na kubeba huzuni zetu.Sisi tulifikiri amepata adhabu,amepigwa na Mungu na kuteswa.

5. Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu,aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu.Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai;kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6. Sisi sote tumepotea kama kondoo,kila mmoja wetu ameelekea njia yake.Lakini Mwenyezi-Mungu alimtwika adhabu,ambayo sisi wenyewe tuliistahili.

7. Alidhulumiwa na kuteswa,lakini alivumilia kwa unyenyekevu,bila kutoa sauti hata kidogo.Alikuwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni,kama kondoo akaavyo kimya anapokatwa manyoya.Hakutoa sauti hata kidogo.

8. Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa;na hakuna mtu aliyejali yanayompata.Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai,kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

9. Walimzika pamoja na wahalifu;katika kifo aliwekwa pamoja na matajiri,ingawa hakutenda ukatili wowote,wala hakusema neno lolote la udanganyifu.

10. Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumizana kumweka katika huzuni.Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi.Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa;ataishi maisha marefu.Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Isaya 53