Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 7:22-30 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Efraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na ndugu zake wakaja kumfariji.

23. Ndipo Efraimu akalala na mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana. Efraimu akampa jina Beria, kwa sababu ya maafa yaliyoipata jamaa yake.

24. Efraimu alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-horoni ya juu na chini, na Uzen-sheera.

25. Efraimu alimzaa pia Refa ambaye alimzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,

26. Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama,

27. Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.

28. Milki zao na makao yao yalikuwa: Betheli na vitongoji vyake, Naraani uliokuwa upande wa mashariki, Gezeri uliokuwa upande wa magharibi pamoja na vitongoji vyake, Shekemu na vitongoji vyake, na Aya na vitongoji vyake.

29. Na pia mipakani mwa wana wa Manase: Beth-sheani na vitongoji vyake, Taanaki na vitongoji vyake, Megido na vitongoji vyake na Dori na vitongoji vyake. Hiyo ndiyo miji walimoishi wazawa wa Yosefu, mwana wa Israeli.

30. Hawa ndio wazawa wa Asheri. Asheri alikuwa na wana wanne: Imna, Ishva, Ishri na Beria, na binti mmoja jina lake Sera.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 7