Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 7:14-29 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Manase alikuwa na wana wawili kutokana na suria wake Mwaramu: Asrieli na Makiri. Makiri alikuwa baba yake Gileadi.

15. Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake.

16. Maaka mkewe Makiri, alizaa mwana jina lake Pereshi. Jina la nduguye Pereshi lilikuwa Shereshi. Wanawe Shereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.

17. Rakemu alimzaa Bedani. Hawa wote ni wazawa wa Gileadi, mwana wa Makiri, mjukuu wa Manase.

18. Hamo-lekethi, dada yake Gileadi, aliwazaa Ishhodi, Abiezeri na Mala.

19. Wana wa Shemida walikuwa Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.

20. Hawa ndio wazawa wa Efraimu kutoka kizazi hadi kizazi: Shuthela, Beredi, Tahathi, Eleada, Tahathi,

21. Zabadi na Shuthela. Mbali na Shuthela, Efraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa nchi ya Gathi kwa sababu walikwenda huko kuwanyanganya mifugo yao.

22. Efraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na ndugu zake wakaja kumfariji.

23. Ndipo Efraimu akalala na mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana. Efraimu akampa jina Beria, kwa sababu ya maafa yaliyoipata jamaa yake.

24. Efraimu alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-horoni ya juu na chini, na Uzen-sheera.

25. Efraimu alimzaa pia Refa ambaye alimzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,

26. Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama,

27. Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.

28. Milki zao na makao yao yalikuwa: Betheli na vitongoji vyake, Naraani uliokuwa upande wa mashariki, Gezeri uliokuwa upande wa magharibi pamoja na vitongoji vyake, Shekemu na vitongoji vyake, na Aya na vitongoji vyake.

29. Na pia mipakani mwa wana wa Manase: Beth-sheani na vitongoji vyake, Taanaki na vitongoji vyake, Megido na vitongoji vyake na Dori na vitongoji vyake. Hiyo ndiyo miji walimoishi wazawa wa Yosefu, mwana wa Israeli.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 7