1. Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake,mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.
2. Heri mtu ambaye Mwenyezi-Mungu hamwekei hatia,mtu ambaye hana hila moyoni mwake.
3. Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu,nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.
4. Mchana na usiku mkono wako ulinilemea;nikafyonzwa nguvu zangu,kama maji wakati wa kiangazi.
5. Kisha nilikiri makosa yangu kwako;wala sikuuficha uovu wangu.Nilisema ninakuungamia makosa yangu ee Mwenyezi-Mungu,ndipo nawe ukanisamehe dhambi zangu zote.
6. Kwa hiyo, kila mwaminifu na akuletee maombi;jeshi likaribiapo au mafuriko,hayo hayatamfikia yeye.