Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 4:13-20 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Watu wapatao 40,000 wakiwa na silaha tayari kwa vita walipita mbele ya Mwenyezi-Mungu wakielekea bonde la mji wa Yeriko.

14. Katika siku hiyo Mwenyezi-Mungu akamtukuza Yoshua mbele ya Waisraeli wote, nao wakamheshimu Yoshua maisha yake yote kama walivyomheshimu Mose maishani mwake.

15. Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua,

16. “Waamuru makuhani wanaobeba sanduku la maamuzi, watoke mtoni Yordani.”

17. Basi, Yoshua akawaamuru wale makuhani, “Tokeni mtoni Yordani.”

18. Hao makuhani waliokuwa wamebeba lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu walipotoka katikati ya mto Yordani, na kukanyaga ukingo wa mto, maji ya mto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama kwanza.

19. Waisraeli walivuka mto Yordani katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi huko mjini Gilgali, mashariki ya Yeriko.

20. Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali.

Kusoma sura kamili Yoshua 4