Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 42:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu:

2. “Najua kwamba waweza kila kitu,lolote unalokusudia haliwezi kuzuiliwa.

3. Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga.Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewamambo ya ajabu mno kwanguambayo sikuwa ninayajua.

4. Uliniambia nisikilize nawe utaniambia;kwamba utaniuliza nami nikujibu.

5. Kweli nilikuwa nimesikia habari zako kwa masikio tu,lakini sasa nakuona kwa macho yangu mwenyewe.

6. Kwa hiyo natubu pamoja na kujipaka mavumbi na majivu,najiona mimi mwenyewe kuwa si kitu kabisa.”

7. Mwenyezi-Mungu alipomaliza kuongea na Yobu, alimwambia Elifazi, Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na marafiki zako wawili kwani hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya.

8. Kwa hiyo chukueni mafahali saba na kondoo madume saba, mwende kwa mtumishi wangu Yobu, mkawatoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Naye mtumishi wangu Yobu atawaombeeni, nami nitaisikiliza sala yake na kuacha kuwatenda kulingana na upumbavu wenu; maana hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya.”

Kusoma sura kamili Yobu 42