Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 8:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, mifupa ya wafalme wa Yuda, mifupa ya wakuu wao, mifupa ya makuhani, mifupa ya manabii na mifupa ya wakazi wote wa Yerusalemu itachimbuliwa makaburini mwao.

2. Itaachwa imetandazwa mbele ya jua na mwezi na sayari zote za mbinguni, vitu ambavyo walivipenda na kuvitumikia, wakavitaka shauri na kuviabudu. Mifupa hiyo haitakusanywa wala kuzikwa, bali itakuwa kama mavi juu ya ardhi.

3. Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

4. “Wewe Yeremia utawaambiakuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mtu akianguka, je hainuki tena?Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?

Kusoma sura kamili Yeremia 8