Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 51:58-64 Biblia Habari Njema (BHN)

58. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa Majeshi nasema:Ukuta mpana wa Babuloniutabomolewa mpaka chini,na malango yake marefuyatateketezwa kwa moto.Watu wanafanya juhudi za bure,mataifa yanajichosha maana mwisho wao ni motoni!”

59. Mnamo mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Sedekia alikwenda Babuloni pamoja na ofisa wa askari wake aitwaye Seraya mwana wa Neria na mjukuu wa Maseya. Kutokana na fursa hiyo mimi Yeremia nilimpa Seraya ujumbe.

60. Nilikuwa nimeandika kitabuni maafa yote niliyotangaza juu ya Babuloni na pia maneno mengine kuhusu Babuloni.

61. Nilimwambia Seraya: “Utakapofika Babuloni ni lazima uwasomee wote ujumbe huu.

62. Kisha umalizie na maneno haya: ‘Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umesema kwamba utapaharibu mahali hapa hata pasikaliwe na kiumbe chochote, mwanadamu au mnyama, na kwamba nchi hii itakuwa jangwa milele.’

63. Utakapomaliza kusoma kitabu hiki, kifungie jiwe, kisha ukitumbukize katikati ya mto Eufrate, ukisema:

64. ‘Hivi ndivyo mji wa Babuloni utakavyozama, wala hautainuka tena, kwa sababu ya maafa ambayo Mwenyezi-Mungu anauletea.’” Mwisho wa maneno ya Yeremia.

Kusoma sura kamili Yeremia 51