Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 5:18-30 Biblia Habari Njema (BHN)

18. “Lakini, hata katika siku hizo mimi Mwenyezi-Mungu nasema, sitawaangamiza na kuwamaliza kabisa.

19. Na watu wenu watakapouliza ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametutendea mambo hayo yote?’ Wewe utawaambia, ‘Nyinyi mlimwacha Mwenyezi-Mungu, mkaitumikia miungu ya kigeni katika nchi yenu. Basi ndivyo mtakavyowatumikia watu wengine katika nchi isiyo yenu.’

20. “Watangazie wazawa wa Yakobo,waambie watu wa Yuda hivi:

21. Sikilizeni enyi wajinga na wapumbavu;watu mlio na macho, lakini hamwoni,mlio na masikio, lakini hamsikii.

22. Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu!Kwa nini hamtetemeki mbele yangu?Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari,kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka.Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita;ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.

23. Lakini watu hawa wana moyo wa ukaidi na uasi;wameniacha wakaenda zao.

24. Wala hawasemi mioyoni mwao;‘Na tumche Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,anayetujalia mvua kwa wakati wake,anayetupatia mvua za masika na mvua za vuli;na kutupa majira maalumu ya mavuno.’

25. Makosa yenu yamewazuia msipate baraka hizo,dhambi zenu zimewafanya msipate mema.

26. Naam, kuna walaghai miongoni mwa watu wangu,watu ambao hunyakua mali za wengine.Wako kama wawindaji wa ndege:Hutega mitego yao na kuwanasa watu.

27. Kama vile kapu lililojaa ndege walionaswa,ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu.Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri,

28. wamenenepa na kunawiri.Katika kutenda maovu hawana kikomohawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa,wala hawatetei haki za watu maskini.

29. “Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya?Je nitaacha kulipiza kisasi taifa kama hili?

30. Jambo la ajabu na la kuchukizalimetokea katika nchi hii:

Kusoma sura kamili Yeremia 5