Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 46:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Misri ni kama mtamba mzuri wa ng'ombe,lakini kipanga kutoka kaskazini amemvamia.

21. Hata askari wake wa kukodiwa ni kama ndama wanono;nao pia wamegeuka, wakakimbia pamoja,wala hawakuweza kustahimili,kwa maana siku yao ya kuangamizwa imefika,wakati wao wa kuadhibiwa umewadia.

22. Misri anatoa sauti kama nyoka anayekimbia;maana maadui zake wanamjia kwa nguvu,wanamjia kwa mashoka kama wakata-miti.

23. Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.

24. Watu wa Misri wataaibishwa,watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.”

25. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: “Tazama, mimi nitamwadhibu Amoni mungu wa Thebesi, nitaiadhibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwadhibu Farao na wote wanaomtegemea.

26. Nitawatia mikononi mwa wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babuloni na maofisa wake. Baadaye, nchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

27. “Lakini wewe usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,usifadhaike, ee Israeli;maana, kutoka mbali nitakuokoa,nitakuja kuwaokoa wazawa wakokutoka nchi walimohamishwa.Yakobo utarudi na kutulia na kustarehe,wala hakuna yeyote atakayekutia hofu.

Kusoma sura kamili Yeremia 46