Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 41:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mnamo mwezi wa saba, Ishmaeli mwana wa Nethania, mjukuu wa Elishama, wa ukoo wa kifalme, mmoja wa maofisa wakuu wa mfalme, alifika Mizpa kwa Gedalia akiandamana na watu kumi. Wakati walipokuwa wanakula chakula huko Mizpa,

2. Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi, wakainuka na kumshambulia kwa upanga Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, wakamuua. Gedalia ndiye aliyekuwa ameteuliwa na mfalme wa Babuloni kuwa mtawala wa nchi.

3. Ishmaeli aliwaua pia Wayahudi wote waliokuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na wanajeshi Wakaldayo waliokuwa mahali hapo.

4. Siku moja baada ya kumwua Gedalia,

5. kabla hata mtu yeyote hajajua habari hizo, walifika watu themanini kutoka Shekemu, Shilo na Samaria. Walikuwa wamenyoa ndevu zao na wamevaa mavazi yaliyotatuka na miili yao imechanjwachanjwa. Walileta tambiko za nafaka na ubani zitolewe hekaluni kwa Mwenyezi-Mungu.

6. Ishmaeli mwana wa Nethania, alitoka nje ya mji kuwalaki watu hao huku analia. Alipokutana nao, akawaambia, “Karibuni nyumbani kwa Gedalia mwana wa Ahikamu.”

7. Walipoingia mjini, Ishmaeli mwana wa Nethania, pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye, waliwaua watu hao na kuzitupa maiti zao kisimani.

Kusoma sura kamili Yeremia 41