Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 4:6-14 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Twekeni bendera ya vita kuelekea Siyoni,kimbilieni usalama wenu, msisitesite!Mwenyezi-Mungu analeta maafana maangamizi makubwa kutoka kaskazini.

7. Kama simba atokavyo mafichoni mwake,mwangamizi wa mataifa ameanza kuja,anakuja kutoka mahali pake,ili kuiharibu nchi yako.Miji yako itakuwa magofu matupu,bila kukaliwa na mtu yeyote.

8. Kwa hiyo, vaa vazi la gunia,omboleza na kulia;maana, hasira kali ya Mwenyezi-Mungu,bado haijaondoka kwetu.

9. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”

10. Kisha nikasema: “Aa, Mwenyezi-Mungu, hakika umewadanganya kabisa watu hawa na mji wa Yerusalemu! Uliwaambia mambo yatawaendea vema, kumbe maisha yao yamo hatarini kabisa!”

11. Wakati huo, wataambiwa hivi watu hawa pamoja na mji wa Yerusalemu, “Upepo wa hari kutoka vilele vikavu vya jangwani utawavumia watu wangu. Huo si upepo wa kupepeta au kusafisha,

12. bali ni upepo mkali sana utokao kwangu. Ni mimi Mwenyezi-Mungu nitakayetoa hukumu juu yao.”

13. Tazama! Adui anakuja kama mawingu.Magari yake ya vita ni kama kimbunga,na farasi wake waenda kasi kuliko tai.Ole wetu! Tumeangamia!

14. Yerusalemu, yasafishe maovu moyoni mwako,ili upate kuokolewa.Mpaka lini utaendelea kuwaza maovu?

Kusoma sura kamili Yeremia 4