Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 22:6-21 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu ikulu ya mfalme wa Yuda:“Ingawa waonekana kuwa mzuri kama nchi ya Gileadikama kilele cha Lebanoni,Lakini naapa kuwa nitakufanya uwe jangwa,uwe mji usiokaliwa na watu.

7. Nitawatayarisha waangamizi dhidi yako,kila mmoja na silaha yake mkononi.Wataikata mierezi yako mizuri,na kuitumbukiza motoni.

8. “Kisha watu wengi wa mataifa watapita karibu na mji huu, na kila mmoja atamwuliza mwenzake: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameutenda hivi mji huu mkubwa?’

9. Wenzao watawajibu, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaiabudu miungu mingine na kuitumikia.’”

10. Msimlilie mtu aliyekufa,wala msiombolezee kifo chake.Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.

11. Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Shalumu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyetawala baada ya Yosia baba yake, na ambaye aliondoka mahali hapa: “Shalumu hatarudi tena mahali hapa,

12. bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii.

13. “Ole wako Yehoyakimuwewe unayejenga nyumba kwa dhulumana kuiwekea ghorofa bila kutumia haki.Unawaajiri watu wakutumikie burewala huwalipi mishahara yao.

14. Wewe wasema:‘Nitalijenga jumba kubwa,lenye vyumba vikubwa ghorofani.’Kisha huifanyia madirisha,ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi,na kuipaka rangi nyekundu!

15. Unadhani umekuwa mfalmekwa kushindana kujenga kwa mierezi?Baba yako alikula na kunywa,akatenda mambo ya haki na memandipo mambo yake yakamwendea vema.

16. Aliwapatia haki maskini na wahitaji,na mambo yake yakamwendea vema.Hii ndiyo maana ya kunijua mimi Mwenyezi-Mungu.

17. Lakini macho yako wewe na moyo wako,hungangania tu mapato yasiyo halali.Unamwaga damu ya wasio na hatia,na kuwatendea watu dhuluma na ukatili.

18. “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:Wakati atakapokufa,hakuna atakayemwombolezea akisema,‘Ole, kaka yangu!’‘Ole, dada yangu!’Hakuna atakayemlilia akisema,‘Maskini, bwana wangu!’‘Maskini, mfalme wangu!’

19. Atazikwa bila heshima kama punda,ataburutwa na kutupiliwa mbali,nje ya malango ya Yerusalemu.”

20. Enyi watu wa Yerusalemu,pandeni Lebanoni mpige kelele,pazeni sauti zenu huko Bashani;lieni kutoka milima ya Abarimu,maana wapenzi wenu wote wameangamizwa.

21. Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi mlipokuwa na fanaka,lakini nyinyi mkasema, “Hatutasikiliza.”Hii ndiyo tabia yenu tangu ujana wenu,hamjapata kuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Yeremia 22