Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 22:23-30 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Enyi wakazi wote wa Lebanoni,nyinyi mkaao salama kati ya mierezi;jinsi gani mtakavyopiga kite uchungu utakapowakumba,uchungu kama wa mama anayejifungua!

24. Na kuhusu Konia mfalme wa Yuda, mwanawe Yehoyakimu, Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu kwamba hata kama wewe Konia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekuvulia mbali.

25. Nitakutia mikononi mwa wale wanaotaka kuyamaliza maisha yako; naam, mikononi mwa wale unaowaogopa, mikononi mwa Nebukadneza, mfalme wa Babuloni; naam, mikononi mwa Wakaldayo.

26. Nitakufukuzia mbali katika nchi ya kigeni, wewe pamoja na mama yako mzazi. Mtakuwa watumwa katika nchi hiyo ambamo nyote wawili hamkuzaliwa, nanyi mtafia hukohuko.

27. Mtatamani kwa hamu kubwa kurudi katika nchi hii, lakini hamtarudi kamwe.

28. Je, huyu mtu Konia,amekuwa kama chungu kilichovunjika,ambacho hudharauliwa na kutupwa nje?Kwa nini yeye na watoto wake wametupwa mbaliwakatupwa katika nchi wasiyoijua?

29. Ee nchi, ee nchi, ee nchi!Sikia neno la Mwenyezi-Mungu!

30. Mwenyezi-Mungu asema hivi:Mwandike mtu huyu kwamba hana watoto,mtu ambaye hatafanikiwa maishani mwake.Maana hakuna hata mmoja wa wazawa wakeatakayekikalia kiti cha enzi cha Daudina kutawala tena katika Yuda.

Kusoma sura kamili Yeremia 22