Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 22:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nenda katika ikulu ya mfalme wa Yuda, uwape watu ujumbe huu:

2. Wewe mfalme wa Yuda unayekikalia kiti cha enzi cha mfalme Daudi, pamoja na watumishi wako na watu wako wanaopita katika malango haya, sikilizeni neno langu mimi Mwenyezi-Mungu.

3. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tendeni mambo ya haki na uadilifu. Mwokoeni mikononi mwa mdhalimu mtu yeyote aliyenyanganywa mali zake. Msiwatendee vibaya au ukatili wageni, yatima na wajane wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa.

4. Kama mkishika neno hili nililowaambia basi, wafalme wanaokikalia kiti cha enzi cha Daudi wataendelea kuingia kwa kupitia malango ya ikulu hii. Watapita pamoja na watumishi wao na watu wao, wakiwa wamepanda farasi na magari ya farasi.

5. Lakini kama hamtatii maneno haya, mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwa nafsi yangu kwamba mahali hapa patakuwa magofu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

6. Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu ikulu ya mfalme wa Yuda:“Ingawa waonekana kuwa mzuri kama nchi ya Gileadikama kilele cha Lebanoni,Lakini naapa kuwa nitakufanya uwe jangwa,uwe mji usiokaliwa na watu.

7. Nitawatayarisha waangamizi dhidi yako,kila mmoja na silaha yake mkononi.Wataikata mierezi yako mizuri,na kuitumbukiza motoni.

8. “Kisha watu wengi wa mataifa watapita karibu na mji huu, na kila mmoja atamwuliza mwenzake: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameutenda hivi mji huu mkubwa?’

9. Wenzao watawajibu, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaiabudu miungu mingine na kuitumikia.’”

10. Msimlilie mtu aliyekufa,wala msiombolezee kifo chake.Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.

11. Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Shalumu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyetawala baada ya Yosia baba yake, na ambaye aliondoka mahali hapa: “Shalumu hatarudi tena mahali hapa,

12. bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii.

13. “Ole wako Yehoyakimuwewe unayejenga nyumba kwa dhulumana kuiwekea ghorofa bila kutumia haki.Unawaajiri watu wakutumikie burewala huwalipi mishahara yao.

14. Wewe wasema:‘Nitalijenga jumba kubwa,lenye vyumba vikubwa ghorofani.’Kisha huifanyia madirisha,ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi,na kuipaka rangi nyekundu!

Kusoma sura kamili Yeremia 22