Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 16:15-21 Biblia Habari Njema (BHN)

15. bali wataapa kwa kusema, ‘Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu aliyewatoa Waisraeli kutoka nchi ya kaskazini na kutoka katika nchi zote alikowafukuzia!’ Maana, nitawarudisha katika nchi yao niliyowapa wazee wao.”

16. Mwenyezi-Mungu asema: “Tazama, nitaita wavuvi wengi waje kuwakamata watu hawa. Kisha, nitaita wawindaji wengi watakaowawinda katika kila mlima, kila kilima na katika mapango ya miambani.

17. Maana, mimi nayaona matendo yao yote. Hakuna chochote kilichofichika kwangu. Makosa yao yote ni wazi mbele yangu.

18. Nitalipiza kisasi maradufu juu ya dhambi zao na makosa yao kwa sababu wameitia unajisi nchi yangu kwa mizoga ya miungu yao ya kuchukiza, wakaijaza hii nchi yangu machukizo yao.”

19. Ee Mwenyezi-Mungu!Wewe ndiwe nguvu yangu na ngome yangu;wewe ni kimbilio langu wakati wa taabu.Mataifa toka pande zote duniani yatakujia na kusema:“Wazee wetu hawakuwa na kitu ila miungu ya uongo,vitu duni visivyo na faida yoyote.

20. Je, binadamu aweza kujitengenezea miungu?Basi, hao si miungu hata kidogo!”

21. “Kwa hiyo,” asema Mwenyezi-Mungu, “wakati huu nitawafundisha watambue waziwazi nguvu zangu na uwezo wangu, nao watajua kwamba jina langu ni Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Yeremia 16