Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 13:15-26 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Enyi Waisraeli, sikilizeni kwa makini,msiwe na majivuno maana Mwenyezi-Mungu anasema nanyi.

16. Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,kabla hajawaletea giza,nanyi mkajikwaa miguu kwenye milima ya giza.Nyinyi mnatazamia mwanga,lakini anaugeuza kuwa utusitusina kuufanya kuwa giza nene.

17. Lakini kama msiponisikiliza,moyo wangu utalia machozi faraghani,kwa sababu ya kiburi chenu.Nitalia kwa uchungu na kububujika machozi,kwa kuwa watu wa Mwenyezi-Mungu wametekwa.

18. Mwambie mfalme na mama yake hivi:“Shukeni kwenye viti vyenu vya enzi,maana taji zenu nzuri zimeanguka vichwani mwenu.

19. Miji ya Negebu imezingirwa;hakuna awezaye kufungua malango yake.Watu wa Yuda wamechukuliwa mateka,wote kabisa wamepelekwa utumwani.”

20. Inua macho yako, ee Yerusalemu!Tazama! Madui zako waja kutoka kaskazini.Kundi ulilokabidhiwa liko wapi?Kundi lako zuri li wapi?

21. Utasemaje juu ya wale uliodhani ni rafiki,wale ambao wewe mwenyewe uliwafundisha,watakapokushinda na kukutawala?Je, si utakumbwa na uchungukama wa mama anayejifungua?

22. Nawe utajiuliza moyoni mwako,“Kwa nini mambo haya yamenipata?”Sawa! Kama vazi lako limepandishwa juu,nawe ukatendewa kwa ukatili mno,hayo ni matokeo ya makosa yako mengi mno.

23. Je, Mwethiopia aweza kubadili rangi yake,au chui madoadoa yake?Ikiwezekana, nanyi pia mnaweza kutenda mema,nyinyi mliozoea kutenda maovu!

24. Mwenyezi-Mungu atawatawanya kama makapiyanayopeperushwa na upepo kutoka jangwani.

25. Mwenyezi-Mungu asema:“Hayo ndiyo yatakayokupata,ndivyo nilivyoamua kukutenda mimi Mwenyezi-Mungu,kwa sababu umenisahau mimi,ukaamini miungu ya uongo.

26. Nitalipandisha vazi lako hadi kichwanina aibu yako yote itaonekana wazi.

Kusoma sura kamili Yeremia 13