Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 2:2-11 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Kama yungiyungi kati ya michongoma,ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wasichana.

3. Kama mtofaa kati ya miti ya msituni,ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wavulana.Nafurahia kuketi chini ya kivuli chake,na tunda lake tamu sana kwangu.

4. Alinichukua hadi ukumbi wa karamu,akatweka bendera ya mapenzi juu yangu.

5. Nishibishe na zabibu kavu,niburudishe kwa matofaa,maana naugua kwa mapenzi!

6. Mkono wake wa kushoto chini ya kichwa changu,mkono wake wa kulia wanikumbatia.

7. Nawasihi enyi wanawake wa Yerusalemu,kama walivyo paa au swala wa porini,msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,hadi hapo wakati wake utakapofika.

8. Hiyo ni sauti ya mpenzi wangu,yuaja mbio,anaruka milima,vilima anavipita kasi!

9. Mpenzi wangu ni kama paa,ni kama swala mchanga.Amesimama karibu na ukuta wetu,achungulia dirishani,atazama kimiani.

10. Mpenzi wangu aniambia:“Inuka basi, ewe mpenzi wangu, unipendezaye,njoo twende zetu.

11. Tazama, majira ya baridi yamepita,nazo mvua zimekwisha koma;

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 2