Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 1:7-16 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Hebu niambie ee wangu wa moyo,utawalisha wapi kondoo wako?Ni wapi watakapopumzikia adhuhuri?Kwa nini mimi nikutafutekati ya makundi ya wenzako?

8. Ewe upendezaye kuliko wanawake wote;kama hujui, fanya hivi:Zifuate nyayo za kondoo;basi, walishe mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.

9. Wewe ee mpenzi wangu,nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao.

10. Mashavu yako yavutia kwa vipuli,na shingo yako kwa mikufu ya johari.

11. Lakini tutakufanyizia mikufu ya dhahabu,iliyopambwa barabara kwa fedha.

12. Mfalme alipokuwa kwenye kochi lake,marashi yangu ya nardo yalisambaa kila mahali.

13. Mpenzi wangu ni kama mfuko wa manemane kwangu,kati ya matiti yangu.

14. Mpenzi wangu ni kama maua ya hina yachanuayo,kwenye mashamba ya mizabibu huko Engedi.

15. Hakika u mzuri, ee mpenzi wangu,hakika u mzuri!Macho yako ni kama ya hua!

16. Hakika u mzuri ewe nikupendaye,u mzuri kweli!Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu;

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 1