Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 1:2-10 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Heri midomo yako inibusu,maana pendo lako ni bora kuliko divai.

3. Manukato yako yanukia vizuri,na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa.Kwa hiyo wanawake hukupenda!

4. Nichukue, twende zetu haraka,mfalme amenileta katika chumba chake.Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako,tutasifu mapenzi yako kuliko divai.Wanawake wana haki kukupenda!

5. Enyi wanawake wa Yerusalemu,mimi ni mweusi na ninapendeza,kama mahema ya Kedari,kama mapazia ya Solomoni.

6. Msinishangae kwa sababu ni mweusi,maana jua limenichoma.Ndugu zangu walinikasirikia,wakanifanya mlinzi wa mashamba ya mizabibu.Lakini sikutunza shamba langu la mizabibu.

7. Hebu niambie ee wangu wa moyo,utawalisha wapi kondoo wako?Ni wapi watakapopumzikia adhuhuri?Kwa nini mimi nikutafutekati ya makundi ya wenzako?

8. Ewe upendezaye kuliko wanawake wote;kama hujui, fanya hivi:Zifuate nyayo za kondoo;basi, walishe mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.

9. Wewe ee mpenzi wangu,nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao.

10. Mashavu yako yavutia kwa vipuli,na shingo yako kwa mikufu ya johari.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 1