Agano la Kale

Agano Jipya

Walawi 13:34-42 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Siku ya saba, kuhani ataviangalia vile vipele. Iwapo kuhani ataona kuwa vipele hivyo havikuenea kwenye ngozi na wala havikwenda ndani ya ngozi, basi, atamtangaza mtu huyo kuwa safi. Mtu huyo atafua mavazi yake, naye atakuwa safi.

35. Lakini iwapo vipele hivyo vimeenea baada ya kutakaswa,

36. mtu huyo ataangaliwa na kuhani na ikiwa vimeenea kwenye ngozi, kuhani hatahitaji kutafuta nywele zenye rangi manjano; mtu huyo atakuwa najisi.

37. Lakini iwapo kuhani ataona kuwa vile vipele vimepona na nywele nyeusi zimeota mahali hapo, basi, vidonda hivyo vimepona, basi, mtu huyo ni safi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa safi.

38. “Kama mtu yeyote, awe mwanamume au mwanamke, ana alama nyeupe mwilini mwake,

39. kuhani atamwangalia mtu huyo. Iwapo kuhani ataona kuwa alama hizo ni nyeupe kiasi, huo ni upele wa kawaida; mtu huyo ni safi.

40. “Kama mwanamume amepata upara, yeye ni safi kwani ana upara tu.

41. Iwapo upara huo umetanda tangu nyuma mpaka mbele mtu huyo ana upara tu na yu safi.

42. Lakini kama kwenye kichwa penye upara au kwenye paji la uso penye upara kuna alama nyekundu-nyeupe, huo ni ukoma unaotokea kwenye upara wake kichwani au kwenye paji lake.

Kusoma sura kamili Walawi 13