Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 5:6-18 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi,katika wakati wa Yaeli,misafara ilikoma kupita nchini,wasafiri walipitia vichochoroni.

7. Wakulima walikoma kuwako,walikoma kuwako katika Israeli,mpaka nilipotokea mimi Debora,mimi niliye kama mama wa Israeli.

8. Walijichagulia miungu mipya,kukawa na vita katika nchi.Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngaokati ya watu 40,000 wa Israeli.

9. Nawapa heshima makamanda wa Israeliwaliojitoa kwa hiari yao kati ya watu.Mshukuruni Mwenyezi-Mungu!

10. “Tangazeni, enyi wapandapunda weupe,enyi mnaokalia mazulia ya fahari,nyinyi mnaotembea njiani, tangazeni jambo hilo.

11. Imbeni kupita wanamuziki kwenye visima vya maji,tangazeni ushindi wa Mwenyezi-Mungu,ushindi kwa wakulima wake katika Israeli.Ndipo watu wa Mwenyezi-Mungu waliposhuka malangoni.

12. “Amka, amka, Debora!Amka! Amka uimbe wimbo!Amka, Baraki mwana wa Abinoamu,uwachukue mateka wako.

13. Mashujaa waliobaki waliteremka,watu wa Mwenyezi-Mungu walikwenda kumpiganiadhidi ya wenye nguvu.

14. Kutoka Efraimu waliteremka bondeni,wakafuata ndugu zao watu wa Benyamini;kutoka Makiri walishuka makamanda,kutoka Zebuluni maofisa wakuu.

15. Wakuu wa Isakari wakafuatana na Debora,watu wa Isakari waaminifu kwa Baraki;wakamfuata mbio mpaka bondeni.Lakini miongoni mwa koo za Reubenikulikuwamo kusitasita kwingi.

16. Kwa nini walibaki mazizini?Ili kusikiliza milio ya kondoo?Miongoni mwa koo za Reubenikulikuwamo kusitasita kwingi.

17. Kabila la Gileadi lilibaki ngambo ya Yordani.Kabila la Dani, kwa nini mlibaki merikebuni?Kabila la Asheri lilitulia huko pwani ya bahari,lilikaa bandarini mwake.

18. Watu wa Zebuluni ni watuwaliohatarisha maisha yao katika kifo.Hata wa Naftali walikikabili kifokwenye miinuko ya mashamba.

Kusoma sura kamili Waamuzi 5