Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 9:21-27 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Ukawatunza jangwani kwa miaka arubainina hawakukosa chochote;mavazi yao hayakuchakaawala nyayo zao hazikuvimba.

22. “Ukawaruhusu kushinda falme na mataifa,ukawafanyia mengi kila upande.Wakaishinda nchi ya Heshbonialikotawala mfalme Sihoni;na tena wakaishinda nchi ya Bashanialikotawala mfalme Ogu.

23. Wazawa wao ukawafanya wawe wengikama nyota za mbinguni;ukawaleta katika nchiuliyowaahidi babu zao.

24. Hivyo, hao wazawa wakaja na kuimiliki nchi;uliwashinda wakazi wa nchi hiyo,Wakanaani, ukawatia mikononi mwao,pamoja na wafalme wao,watu wao na nchi yao ili wawatende wapendavyo.

25. Miji yenye ngome wakaiteka,wakachukua nchi yenye utajiri,majumba yenye vitu vingi vizuri,visima vilivyochimbwa,mashamba ya mizabibu na mizeitunipamoja na miti yenye matunda kwa wingi.Hivyo wakala,wakashiba na kunenepana kuufurahia wema wako.

26. Lakini hawakuwa waaminifu kwako.Wakakuasi,wakaiacha sheria yakona kuwaua manabii waliowaonyaili wakurudie wewe.Wakakufuru sana.

27. Hivyo, ukawatia katika mikono ya adui zao,nao wakawatesa.Lakini wakiwa katika mateso yao,wakakulilia, nawe ukawasikia kutoka mbinguni.Na kwa huruma zako nyingi,ukawapelekea viongozi wa kuwaokoa;nao wakawakomboa toka mikononi mwao.

Kusoma sura kamili Nehemia 9