Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 9:13-22 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kule mlimani Sinaiulishuka toka mbinguni na kuzungumza nao.Ukawapa maagizo safi, sheria za kweli,kanuni nzuri na amri.

14. Kwa njia ya Mose, mtumishi wako,ukawajulisha Sabato yako takatifuna ukawaagiza kuzifuata amri,kanuni na sheria ulizowaamrisha.

15. Walipokuwa na njaa,ukawapa chakula kutoka mbinguni.Walipokuwa na kiuukawapa maji kutoka kwenye mwamba.Ukawaagiza kuichukua nchi uliyokuwa umewaahidi.

16. Lakini wao na babu zetu wakawa na kiburina wakawa na shingo ngumuwakakataa kufuata maagizo yako.

17. Wakakataa kutii;wasiyakumbuke maajabu uliyofanya miongoni mwao.Wakawa na shingo zao ngumu,wakajichagulia kiongozi wa kuwarudishautumwani nchini Misri.Bali wewe Mungu u mwepesi kusamehe,mwenye neema na huruma,wewe hukasiriki upesi.U mwenye fadhili nyingi, na hukuwatupa.

18. Hata walipojitengenezea sanamu ya ndama na kusema,‘Huyu ndiye mungu wetualiyetutoa kutoka nchi ya Misri,’wakawa wamefanya kufuru kubwa.

19. Wewe kwa huruma zako nyingihukuwatupa kule jangwani.Mnara wa winguuliowaongoza mchana haukuondoka,wala mnara wa motouliowamulikia njia usiku, haukuondoka.

20. Ukawapa roho yako njema kuwashauri;ukawapa mana kuwa chakula chao na maji ya kunywaili kutuliza kiu chao.

21. Ukawatunza jangwani kwa miaka arubainina hawakukosa chochote;mavazi yao hayakuchakaawala nyayo zao hazikuvimba.

22. “Ukawaruhusu kushinda falme na mataifa,ukawafanyia mengi kila upande.Wakaishinda nchi ya Heshbonialikotawala mfalme Sihoni;na tena wakaishinda nchi ya Bashanialikotawala mfalme Ogu.

Kusoma sura kamili Nehemia 9