Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 5:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Hivyo Mungu atawaacha watu wake kwa maadui,mpaka yule mama mjamzito atakapojifungua.Kisha ndugu zake waliobakia,watarudi na kuungana na Waisraeli wenzao.

4. Huyo mtawala atawachunga watu wake kwa nguvu ya Mwenyezi-Mungu,kwa fahari yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.Watu wake wataishi kwa usalama,maana atakuwa mkuu mpaka miisho ya dunia.

5. Yeye ndiye atakayeleta amani.Waashuru wakivamia nchi yetu,na kuupenya ulinzi wetu,tutapeleka walinzi wawakabili,naam, tutawapeleka viongozi wetu kwa wingi.

6. Kwa silaha zao wataitawala nchi ya Ashuru,na kuimiliki nchi ya Nimrodi.Watatuokoa mikononi mwa Waashuru,watakapowasili mipakani mwa nchi yetuna kuanza kuivamia nchi yetu.

7. Wazawa wa Yakobo watakaobaki haiwameenea miongoni mwa mataifa mengi,watakuwa kama umande wa Mwenyezi-Mungu uburudishao,kama manyunyu yaangukayo penye nyasiambayo hayasababishwi na mtuwala kumtegemea binadamu.

Kusoma sura kamili Mika 5