Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 2:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ole wao wanaopanga kutenda maovuwanaolala usiku wakiazimia uovu!Mara tu kunapopambazuka,wanayatekeleza kwani wanao uwezo.

2. Hutamani mashamba na kuyatwaa;wakitaka nyumba, wananyakua.Huwadhulumu wenye nyumba na jamaa zao,huwanyang'anya watu mali zao.

3. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Ninapanga kuwaleteeni nyinyi maafa,ambayo kamwe hamtaweza kuyakwepa.Utakuwa wakati mbaya kwenu,wala hamtaweza kwenda kwa maringo.

4. Siku hiyo watu watawasimanga kwa wimbo,watalia na kuomboleza kwa uchungu, wakisema:‘Tumeangamia kabisa;Mwenyezi-Mungu amechukua nchi yetu,naam, ameiondoa mikononi mwetu.Mashamba yetu amewagawia waliotuteka.’”

5. Kwa hiyo hamtagawiwa sehemu yoyote ya ardhimiongoni mwa watu wake Mwenyezi-Mungu.

6. “Usituhubirie sisi.Mambo kama hayo si ya kuhubiriwa.Sisi hatutakumbwa na maafa!

7. Je, yafaa kusema hivyo, wazawa wa Yakobo?Je, Mwenyezi-Mungu ameacha uvumilivu wake?Je, yeye hufanya mambo kama haya?”Sivyo! Maneno yangu huwafaa watendao mambo mema.

8. Lakini Mwenyezi-Mungu awaambia hivi:“Nyinyi mnawavamia watu wangu kama adui.Mnawanyang'anya mavazi yao watu watulivu;watu wanaopita kwenda zao bila wasiwasi,na wasio na fikira zozote za vita.

9. Mnawafukuza wake za watu wangukutoka nyumba zao nzuri;watoto wao mmewaondolea fahari yangu milele.

10. Inukeni mwende zenu!Hapa hamna tena pa kupumzika!Kwa utovu wenu wa uaminifumaangamizi makubwa yanawangojea!

Kusoma sura kamili Mika 2