Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 1:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Mika, mwenyeji wa Moreshethi, wakati Yothamu, Ahazi na Hezekia walipokuwa wafalme wa Yuda. Mika aliona mambo yote haya kuhusu Samaria na Yerusalemu.

2. Sikilizeni enyi watu wote;sikiliza ewe dunia na vyote vilivyomo.Mwenyezi-Mungu anakuja kuwashtaki,Bwana anena kutoka hekalu lake takatifu.

3. Naam! Mwenyezi-Mungu yuaja kutoka makao yake;atashuka na kutembea juu ya vilele vya dunia.

4. Milima itayeyuka chini ya nyayo zake,kama nta karibu na moto;mabonde yatapasuka,kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.

5. Haya yote yatatukiakwa sababu ya makosa ya wazawa wa Yakobo,kwa sababu ya dhambi za wazawa wa Israeli.Je, uhalifu wa Yakobo waonekana wapi?Katika mji wake mkuu Samaria!Je, uhalifu wa Yuda waonekana wapi?Katika Yerusalemu kwenyewe!

6. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mji wa Samaria nitaufanya magofu nyikani,shamba ambalo watu watapanda mizabibu.Mawe yaliyoujenga nitayatupa bondeni,na misingi yake nitaichimbuachimbua.

7. Sanamu zake zote zitavunjwavunjwa,kila kilichochumwa kitateketezwa kwa moto.Vinyago vyake vyote nitaviharibu.Vilirundikwa kutokana na ujira wa malaya,navyo vitatumiwa tena kulipia umalaya.”

8. Kwa sababu hiyo, mimi nitalia na kuomboleza;nitatembea uchi na bila viatu.Nitaomboleza na kulia kama mbweha,nitasikitika na kulia kama mbuni.

Kusoma sura kamili Mika 1