Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12

Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 7 Biblia Habari Njema (BHN)

Mawaidha kuhusu maisha

1. Sifa njema ni bora kuliko marashi ya thamani.Siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.

2. Afadhali kwenda kwenye matanga,kuliko kwenda kwenye karamu,kwa sababu walio hai yawapasa kukumbuka kwamba kifo chatungojea sisi sote.

3. Huzuni ni afadhali kuliko kichekomaana, huzuni ya uso ni faida ya moyo.

4. Moyo wa mwenye hekima huthamini matanga,lakini moyo wa mpumbavu hupenda raha.

5. Afadhali kusikia maonyo ya wenye hekimakuliko kusikiliza nyimbo za wapumbavu.

6. Maana, kicheko cha mpumbavuni kama mlio wa miiba motoni.Hayo nayo ni bure kabisa.

7. Mwenye hekima akimdhulumu mtu;hujifanya mwenyewe kuwa mpumbavukupokea rushwa hupotosha akili.

8. Mwisho wa jambo ni afadhali kuliko mwanzo wake;mvumilivu rohoni ni bora kuliko mwenye majivuno.

9. Usiwe mwepesi wa hasira,maana, hasira hukaa ndani ya wapumbavu.

10. Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?”Huulizi hivyo kwa kutumia hekima.

11. Hekima ni ya thamani kubwa kama urithi;ni muhimu kwa wale wote walio hai.

12. Kulindwa na hekima ni kama kulindwa na fedha.Faida ya maarifa ni kwamba hekima hulinda maisha ya mtu aliye nayo.

13. Tafakarini vema kazi yake Mungu;ni nani awezaye kunyosha alichopinda Mungu?

14. Katika siku za fanaka uwe na furaha; katika siku za maafa utafakari jambo hili: Fanaka, pia maafa, Mungu amefanya hiyo ya kwanza iambatane na ya pili ili binadamu asiweze kujua yatakayotukia baada yake.

15. Katika maisha yangu duni, nimeona kila kitu; mtu mwadilifu hufa ingawa ni mwadilifu, ambapo mtu mwovu huendelea kuishi maisha marefu ingawa ni mwovu.

16. Basi, usiwe mwadilifu sana, wala usiwe mwenye hekima mno! Ya nini kujiangamiza wewe mwenyewe?

17. Lakini pia, usiwe mwovu sana wala usiwe mpumbavu! Ya nini kufa kabla ya wakati wako?

18. Inakupasa ushike la kwanza na la pili pia; maana anayemtii Mungu atajengwa kwayo.

19. Hekima humfanya mwenye busara kuwa na nguvu zaidi kuliko watawala kumi mjini.

20. Hakika, hakuna mtu mwadilifu duniani atendaye mema daima bila kutenda dhambi.

21. Usitie maanani maneno yote wasemayo wanadamu, usije ukamsikia mtumishi wako akikutukana.

22. Wewe mwenyewe wajua moyoni kwamba umeapiza wengine mara nyingi.

Kuomba hekima

23. Nimeyapima hayo yote kwa hekima; nikajisemea: “Nataka kuwa mwenye hekima!” Lakini hekima iko mbali sana nami.

24. Jinsi gani binadamu ataweza kugundua maana ya maisha; jambo hilo ni zito na gumu mno kwetu!

25. Hata hivyo, nilipania kujua na kuchunguza na kutafuta hekima na maana ya mambo yaliyoko, na pia kujua uovu ni upuuzi, na upumbavu ni wazimu.

26. Jambo moja nililogundua lililo baya zaidi kuliko kifo, ni mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na wavu, na mikono yake ni kama minyororo. Lakini anayempendeza Mungu humkwepa mwanamke huyo, lakini mwenye dhambi hunaswa naye.

27. Haya, nakuambia mimi Mhubiri, ndio niliyogundua nilipofanya uchunguzi wangu kidogokidogo.

28. Nilipania kugundua mambo hayo tena na tena, lakini sikufaulu. Kati ya wanaume elfu moja, nilifaulu kumwona mwanamume mmoja, anayestahili heshima, lakini kati ya wanawake wote kama hao sikumwona hata mmoja anayestahili heshima.

29. Tazama, nimegundua jambo hili moja: Kwamba Mungu aliwaumba wanadamu wanyofu, lakini wao wenyewe wamejitafutia matatizo.