Agano la Kale

Agano Jipya

Malaki 2:13-17 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Zaidi ya hayo yote, mnaifunika madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kwa machozi yenu, mkilia na kuomboleza kwa sababu yeye hazikubali tena tambiko mnazomtolea.

14. Mnauliza, “Mbona sasa hazikubali?” Mwenyezi-Mungu hazikubali kwa sababu anajua wazi kuwa umeivunja ahadi yako kwa mke wa ujana wako. Umekosa uaminifu kwake ingawa uliahidi mbele ya Mungu kwamba ungekuwa mwaminifu kwake.

15. Je, Mungu hakuwafanya nyote wawili muwe mwili mmoja na roho moja? Je, alikusudia nini alipofanya hayo? Yamkini alikusudia tuzae watoto ambao watamcha yeye. Kwa hiyo, hakikisheni kuwa hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.

16. Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli asema: “Ninachukia talaka. Ninachukia mmoja wenu anapomtendea mkewe ukatili huo. Hakikisheni kwamba hakuna hata mmoja wenu anayekosa uaminifu kwa mkewe.”

17. Mmemchosha Mwenyezi-Mungu kwa maneno yenu matupu. Hata hivyo, mnasema, “Tumemchoshaje?” Mmemchosha mnaposema, “Mwenyezi-Mungu huwaona kuwa wema watu wanaotenda maovu; tena anawapenda.” Au mnapouliza, “Yuko wapi yule Mungu mwenye haki?”

Kusoma sura kamili Malaki 2